Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuisadia Uganda kujenga jumba la kumbukumbu lililoungua

UM kuisadia Uganda kujenga jumba la kumbukumbu lililoungua

Umoja wa Mataifa utaisaidia serikali ya Uganda kukusanya fedha za kukarabati makaburi ya wafalme wa Buganda yaliyoungua mwezi uliopita.

Makaburi hayo ni moja ya maeneo ya urithi wa kimataifa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO umesema jopo la wataalamu waliotathimi athari za moto huo wa Machi 16 wamesema makaburi hayo yanaweza kukarabatiwa.

Makaburi ya wafalme wa Bunganda yapo kwenye eneo la mlima Kasubi kilometa tano kutoka mji mkuu Kampala na yaliteketea sana kwasababu yamejengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi.

Makaburi hayo yaliongezwa kwenye orodha ya UNESCO ya urithi wa kimataifa mwaka 2001 na eneo hilo ni muhimu sana kwa shughuli za kidini kwa Wabaganda tangu lilipojengwa karne ya 19.