Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea mipango ya kuifuatilia baada ya mkutana wa nyuklia wa Washington

Ban aelezea mipango ya kuifuatilia baada ya mkutana wa nyuklia wa Washington

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amependekeza kufanyika mikutano kadhaa ya ngazi za juu ili kuimatisha nia ya kimataifa ya kuzuia ugaidi wa nyuklia.

Ban amesema mkataba wa kimataifa wa kuzuia ugaidi wa nyuklia uliopitishwa miaka mitano iliyopita umeridhia na theluthi tuu ya wanachama wa Umoja wa Mataifa, na amezitolea wito nchi zote ambazo bado hazijaridhia mkataba wa upigaji marufuku majaribio ya nyuklia kufanya hivyo mara moja.