Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR na serikali ya Tanzania wajadili hatma ya wakimbizi wa Burundi

UNHCR na serikali ya Tanzania wajadili hatma ya wakimbizi wa Burundi

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Antonio Guterres yuko nchini Tanzania kutathmini suala la wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi walioko nchini humo.

Bwana Guterres leo amezitembelea kambi za wakimbizi zilizoko Kigoma Magharibi mwa Tanzania ili kutathimini shughuli ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi hao kwa hiyari na pia kwa wakimbizi 160,000 kutoka Burundi waliokaa Tanzania tangu miaka ya 1970 kupewa hadhi ya uraia.

Tanzania imeshawahifadhi wakimbizi laki tano wa Kirundi walioomba hifadhi miaka 1990 lakini idadi kubwa ya wakimbizi hao sasa wamerejea nyumbani tangu mwaka 2002 hadi mwaka jana. Isaac Nantanga ni msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania anafafanua hali ya sasa ya shughuli ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi hao.