Nchi za Afrika zinakutana Kenya kujaribu kupunguza hatari ya kukumbwa na majanga
Wajumbe kutoka nchi 42 za Afrika pamoja na Asia ambayo hukumbwa sana na majanga asilia wameanza mkutano uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Kenya .
Wajumbe 1700 wanaowakilisha serikali, vyombo vya kiuchumi, wahisani, wanazuoni, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali watajadili mambo muhimu kwa hatma ya bara la Afrika. Na katika mkutano huo wa siku tatu pia wataridhia mkakati mpya wa utekelezaji wa kupunguza majanga Afrika na kuchukua hatua madhubuti kwa kipindi walichojiwekea kati ya 2006 hadi 2015.