Skip to main content

Mamia ya watu wafariki dunia kwenye tetemeko la ardhi Uchina

Mamia ya watu wafariki dunia kwenye tetemeko la ardhi Uchina

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.1 vipimo vya richta limelikumba jimbo la Qinghai kaskazini magharibi mwa Uchina karibu na mkoa wa Tibet mapema leo asubuhi kwa saa za Uchina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uchina Xinhua watu 400 wamefariki dunia, 10,000 wamejeruhiwa, asilimia 85 ya nyumba katika kitongoji cha Jiegu zimeporomoka, umeme, maji na njia ya mawasiliano vimekatwa kabisa na watu wengi bado wamefukiwa kwenye kifusi.

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu ICRC nchini Uchina limesema kwa sasa hawaitaji msaada wa kimataifa na shuguli za uokozi zinazofanywa na vikosi vya serikali zinaendelea na idadi ya vifo na waliojeruhiwa inatarajiwa kuongezeka.