Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi wa AU azuru Kaskazini na Magharibi mwa Darfur

Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi wa AU azuru Kaskazini na Magharibi mwa Darfur

Raia wa Sudan wanaendelea kupiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kwa zaidi ya miongo miwili.

Wakati kura hizo zikiendelea leo mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Afrika amezuru maeneo ya Kaskazini na Magharibi mwa Darfur. Wakati wa ziara yake mkuu huyo ambaye ni Rais wa zamani wa Ghana John Kuffuor amekutana na mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID, viongozi wa Sudan wa eneo hilo, na wajumbe wa vyama mbalimbali vya Suda.

Bwana Kufor amesema taswira aloyoipata ni kwamba kwa wale wanaoshiriki mchakato wa kupiga kura na wanaogomea wote wanathamini umuhimu wa uchaguzi huu. Amesema wanaogomea uchaguzi wamekuwa wakilalamikia kutokuwepo kwa usawa baiana ya chama tawala na vya upinzani na mkanganyiko uliojitokeza katika uandikishaji na katika vituo vya kupigia kura. John Kuffuor amesema licha ya yote haya alichokiona ni kwamba uchaguzi huu ni mwanzo muhimu utakaofungua njia ya matumaini kwa hatma ya Sudan