Naibu Katibu Mkuu ahitimisha ziara Haiti kwa kuzuru watoto wa shule

Naibu Katibu Mkuu ahitimisha ziara Haiti kwa kuzuru watoto wa shule

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro leo ametembelea moja ya shule nchini Haiti katika kuhitimisha ziara yake.

Wanafunzi wanarejea mashuleni miezi mitatu baada ya tetemeko la ardhi la Januari 12 lililokatili maisha ya watu wengi na kuwafanya mamilioni kutegemea msaada. Mfumo wa elimu uliharibiwa vibaya na tetemeko hilo lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaisaidia serikali ya Haiti kuwarejesha mashuleni watoto zaidi ya 700,000 .

UNISEF inasema lengo ni kukamilisha idadi hiyo katika kipindi cha miezi miwili ijayo. Asha Rose ambaye amehitimisha ziara yake Haiti leo baada ya kuwepo nchini humo kwa siku mbili alikutana pia na Rais Preval, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada.