Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahitaji dola milioni 12.5 kuwasaidia wakimbizi wa ndani Haiti

UNHCR yahitaji dola milioni 12.5 kuwasaidia wakimbizi wa ndani Haiti

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linaomba kiasi cha dola milioni 12.5 kusaidia watu wanaishi nje ya makambi rasmi nchini Haiti na wale waliokimbilia nchi jirani ya Jamuhuri ya Dominican.

UNHCR imefanya tathimini kubaini mahitaji ya wakimbizi wa ndani nje ya Port-au-Prince na wale waliko kwenye makambi rasmi. Shirika hilo linasema kwa msaada wa fedha hizo litasaidia kuzuia wakimbizi zaidi, au watu kujerea makwao kabla mazingira hayajawa mazuri na salama.

UNHCR pia inalengo la kuwasaidia Wahaiti 60,000 kwa msaada usio wa chakula kwenye eneo la mpakani. Mbali ya hayo shirika hilo litaendelea kusaidia kurejea nyumbani Wahaiti walioruhusiwa kutoka hospitali katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Dominican Republic na wale walio katika hali ngumu ambao wako nchini Haiti.