Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushahidi umeanza kutolewa dhidi ya kesi ya Radovan Karadzic The Hague

Ushahidi umeanza kutolewa dhidi ya kesi ya Radovan Karadzic The Hague

Kiongozi wa zamani wa Bosnia Serbia Radovan Karadzic anakutana uso kwa uso na shahidi wa kwanza wa upande wa mashikata kwenye kesi ya mauaji ya kimbari inyomkabili.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa tena kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague na shahidi wa kwanza ni Ahmet Zulic aliyekuwa mfungwa kwenye mahabusu ya Serbia kaskazini magharibi mwa Bosnia.

Bwana Karadzic ambaye amekuwa akijitetea mwenyewe anatarajiwa kumuhoji shahidi huyo. Karadzic anakanusha mashitaka 11 ya makosa ya uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari. Makosa yote yanahusiana na vita huko Bosnia-Herzegovina katika miaka ya 1990. Upande wa mashitaka unatarajiwa kuwasilisha ushahidi wake kutoka kwa mashahidi 410 katika kipindi cha miezi kadhaa.