Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaitaka Zambia kusitisha kuwarejesha wakimbizi wa Congo DRC

UNHCR yaitaka Zambia kusitisha kuwarejesha wakimbizi wa Congo DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeilalamikia serikali ya Zambia kwa kuwarudisha makwao wakimbizi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kurudishwa kwa wakimbizi hao kumefuatia masuala ya usalama na operesheni za polisi ambazo zilimaliza maandamano ya wakimbizi hao. UNHCR imesema wakimbizi na watu wanaoomba hifadhi wanatakiwa kufuata sheria za Zambia na inakubaliana na serikali kwamba ni muhimu kuhakikisha usalama na utulivu katika makambi ya wakimbizi.

Lakini inasema inadahani waliokosa wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na sio kufukuzwa kwa nguvu kurejeshwa nchini kwao. Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR