Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu watekwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu watekwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Maafisa wanane wa shirika la msalaba mwekundu wametekwa nyara huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wafanyakazi hao ambao saba ni raia wa Congo na mmoja Mswisi walitekwa wiki jana walipokuwa katika shughuli zao za kutoa misaada kwa wakimbizi walioko mkoa wa Kivu ya Kusini. Habari kutoka Congo zinasema wafanyakazi hao wametekwa na wanachama wa kundi la waasi la Mai Mai Yakutumba karibu na mji wa Fizi.

Eneo hilo linajulikana kwa usalama mdogo na chama cha msalaba mwekundu ni moja ya mashirika machache yanayotoa msaada wa chakula na maji kwa maelfu ya wakimbizi. Msemaji wa chama cha msalaba mwekundu mjini Geneva ametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa mateka hao lakini hakusema endapo kuna mawasiliano yoyote na kundi hilo la waasi wa Mai Mai.