Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni miezi mitatu tangu kutokea tetemeko la ardhi nchini Haiti na kuuawa watu wengu

Ni miezi mitatu tangu kutokea tetemeko la ardhi nchini Haiti na kuuawa watu wengu

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA inasema miezi mitatu baada ya tetemeko la ardhi nchini Haiti mamilioni ya watu wameshapata msaada muhimu.

OCHA inasema zaidi ya watu milioni 3.5 wamepokea msaada wa chakula, milioni 1.3 wanapata

mgao wa maji kila siku, na zaidi ya watu milioni 1.3 wamepokea msaada wa malazi.  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema watoto zaidi ya milioni moja wameathirika na tetemeko hilo lakini wengi wamepata msaada, na wengine wameanza kurejea mashuleni japo msaada zaidi unahitajika.

Nalo shirika la afya duniani WHO linasema watu laki tano wamepata chanjo na msaada wa madawa ambayo yanaweza kutibu watu 91,000. Na kama anavyofafanua Paul Garwood wa WHO hata wenye mahitaji maalumu ya kiafya wamesaidiwa.