Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari wanne wa hawajulikani waliko baada ya kutoweka Nyala Darfur

Askari wanne wa hawajulikani waliko baada ya kutoweka Nyala Darfur

Wanajeshi wanne wa kulinda amani wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID kwenye jimbo la Darfur Sudan wametoweka

Wasiwasi unaongezeka juu ya usalama wa askari hao ambao hawajulikani waliko na hakuna aliyewasikia kwa siku ya pili sasa. Mara ya mwisho askari hao walionekana siku ya Jumapili wakati wakipanga timu yao ya doria katika eneo la Nyala mji mkuu wa Darfur Kusini.

UNAMID imetoa taarifa kusema imekusanya kila kinachohitajika katika eneo hilo ili kuwasaka wanajeshi hao na kwamba inashirikiana kwa karibu na serikali ya Sudan na uongozi wa Darfur ili kuhakikisha wanapatikana.