Wadau wa utabiri wa hali ya hewa wanakutana Nairobi nchini Kenya

Wadau wa utabiri wa hali ya hewa wanakutana Nairobi nchini Kenya

Mkutano huo ni wa kwanza kufanyika barani Afrika na unafanyika Nairobi kwa mwaliko wa serikali ya Kenya.

Katika mkutano wao wa wiki moja ulioandaliwa na shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO, wahusika watajadili mada kadhaa ikiwemo umuhimu wa kuzingatia utabiri wa hali ya hewa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Nchi za Afrika ndizo zenye wajumbe wengi katika mkutano huo unaojumuisha pia Umoja wa Afrika AU, Umoja wa Ulaya EU na Benki ya dunia. Kutoka Nairobi mwandishi wetu Jason Nyakundi anaarifu.