Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa utabiri wa hali ya hewa umeanza Nairobi Kenya

Mkutano wa kimataifa wa utabiri wa hali ya hewa umeanza Nairobi Kenya

Mkutano wa kimataifa wa utabiri wa ya hali ya hewa umeanza leo mjini Nairobi nchini Kenya ukihudhuriwa na watu mbalimbali.

Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO kwa mwaliko rasmi wa serikali ya Kenya unahusisha mawziri wa hali ya hewa kutoka kote barani Afrika, Umoja wa Afrika, Bank ya dunia , Umoja wa Ulaya na nchi kadhaa za mabara mengine.

Mkutano huo ni wa kwanza kufanyika barani Afrika na lengo lake ni kuzishawishi serikali kutilia maanani ripoti zinazotolewa na mashirika ya utabiri wa hali ya hewa ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa. Akizungumza katika mkutano huo naiabu waziri wa mazingira wa Kenya Ramadhani Kajembe amesema kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kunahitaji ushirikiano.