Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kuzuru Tanzania

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kuzuru Tanzania

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Antonio Guterres kuzuru nchini Tanzania katika ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia Jumapili.

Nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki inahifadhi wakimbizi karibu laki moja wengi wao wakiwa kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Bwana Guterres atasafiri hadi magharibi mwa Tanzania siku ya Jumatano ijayo na Alhamisi ambako atakutana na baadhi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Pia atatathimini mchakato wa kuwapa uraia Warundi laki moja na sitini ambao wamekuwemo nchini humo tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Tanzania pia imeshawahifadhi wakimbizi Warundi zaidi ya laki tano ambao waliomba ukimbizi katika miaka ya 1990. Lakini idadi kubwa ya wakimbizi hao walirejea nyumbani kati ya mwaka 2002 na mwaka jana