Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 16 baada ya mauaji ya kimbari Rwanda yaendelea kubadilika

Miaka 16 baada ya mauaji ya kimbari Rwanda yaendelea kubadilika

Wiki hii Rwanda, Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla wamekumbuka simanzi iliyosababishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda hapo mwaka 1994.

Watu takribani laki nane waliuawa, na mamilioni wakalazimika kuwa wakimbizi katika nchi mbalimbali. Katika kumbukumbu hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema UM utahakikisha asilani kilichotokea Rwanda hakitokei tena popote duniani.

Rwanda yenyewe imekuwa msitari wa mbele katika kutimiza usemi wa yaliyopita si ndwele bali tugange yajayo, kwa kuhakikisha inashirikiana na jamii ya kimataifa kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wahusika na kurejesha amani na maridhiano Rwanda. Mwandishi wetu wa maziwa makuu anatathmini kumbukumbu hiyo miaka 16 baada ya mauaji.