Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inaunga mkono kampeni ya kuzifanya shule na hospitali mahala salama

WHO inaunga mkono kampeni ya kuzifanya shule na hospitali mahala salama

Shirika la Afya Duniani WHO linaunga mkono kampeni iliyozinduliwa ya kuzifanya shule na hospitali milioni moja kuwa salama.

Lengo la kampeni hiyo ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ilyozinduliwa jana mjini Manila Philipines ni kulinda afya na vifaa vya elimu na majengo yake.

WHO inasema lakini kikubwa zaidi ni kuwalinda mamilioni ya watu ambao wanategemea shule na hospilati hizo kupata elimu na huduma za afya .