Skip to main content

Upungufu wa fedha unatishia hatma ya wagonjwa wa HIV Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Upungufu wa fedha unatishia hatma ya wagonjwa wa HIV Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iko katika hatari ya kukosa dawa za kurefusha maisha kwa wagonjwa wa HIV kwa sababu mradi wa wahisani kuisaidia nchi hiyo unamaliza muda wake.

Wengine waliokuwa wakitoa msaada ni UNITAID ambao walikuwa wakigawa dawa za kurefusha maisha ARV's linaondoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo 2011. Hivyo wanauacha mfuko wa kimataifa Global Fund kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria nchini humo.

Kwa mujibu wa mratibu wa mradi wa HIV/AIDS unaosaidiwa na madaktari wasio na mipaka, Corinne Benazech, asilimia 10 pekee ya watu elfu 35 nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaohitaji ARV's wanaweza kupata dawa hizo.

Amesema sababu kubwa ni ukosefu wa fedha za kufadhili mradi wa ugawaji wa dawa.

Bi Benazech amesema pamoja na kwamba kiwango na ukimwi Congo DRc sio kikubwa sana ukilinganisha na nchi zingine za Afrika nchi hiyo inahitaji msaada hasa kutokana na vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi.