Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wa habari mashariki mwa Congo DRC

UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wa habari mashariki mwa Congo DRC

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lenye kazi ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari leo amelaani mauaji ya mwandishi habari wa kujitegemea wa televisheni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, mwandhishi huyo Patient Chebeya Bankome, maarufu kama Montigomo aliuawa juzi kwa kupigwa risasi na watu watu waliovalia sare za jeshi akiwa nyumbani kwake mjini Ben.

Bankome aliyekuwa na umri wa miaka 35 alikuwa mwandishi na pia mpigapicha za televisheni na amewafanya kazi na vituo mbalimbali vya televisheni katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.