Skip to main content

Wataalamu wanakutana kufikiria athari za kuingia kwenye uchumi unaojali mazingira

Wataalamu wanakutana kufikiria athari za kuingia kwenye uchumi unaojali mazingira

Wataalamu zaidi ya 600 kutoka nchi 75 wanakutana mjini Geneva kujadili athari za kuingia kwenye uchumi unaojali mazingira. Katika mkutano huo wa kila mwaka ulionza leo watazungumzia athari za kijamii na kimazingira na wataangalia sekta tano zilizotajwa kama kitovu cha fursa ya uwekezaji wa uchumi unaojali mazingira.

Sekta hizo ni kilimo, viwanda, utalii miji na usafirishaji. Moja ya malengo muhimu ya mkutano huo ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira UNEP ni kutoa vifaa na njia ambazo zitazisaidia nchi kutathimini na kuchagua ni uwekezaji upi waufuate unaozingatia mazingira.

Mkutano huo wa siku sita unahudhuriwa na wataalamu wa kimataifa, watunga sera za viwandani, serikali, wasaili, mashirika wahisani, mashirika yasiyo ya kiserikali na wanazuoni