Katibu Mkuu wa UM yuko Vienna ambako amekutana na viongozi wa nchi hiyo

8 Aprili 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yuko Vienna Austria ambako amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje anayehusika na masuala ya Ulaya na uhusiano wa kimataifa Michael Spindelegger.

Bwana Ban Ki-moon amesema mkutano wao umekuwa wa mafanikio na wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo juhudi za kuleta amani na usalama. Katika suala hilo wamezungumzia ushiriki wa vikosi vya kulinda amani vya Austria na Ban amewapongeza askari wa kike na wakiume wanaoshiriki operesheni hizo.

Ban amemuomba waziri huyo wa mambo ya nje wa Austria kuishawishi serikali kuongeza idadi ya wanawake polisi katika shughuli za kulinda amani na kusuluhisha migogoro. Mbali ya hayo wamejadili haja ya Austria kuunga mkono juhudi za amani mashariki ya kati na hatua ya Marekani na Urusi kutaka kupunguza silaha za nyuklia

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter