Uchaguzi Sudan lazima uwe huru na haki asema Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Uchaguzi Sudan lazima uwe huru na haki asema Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa pande zote husika nchini Sudan kuhakikisha uchaguzi wa Jumapili unakuwa huru, wa haki na unaostahili.

Wapinzani wanaosusia uchaguzi huo wanasema wanahofia hali ya usalama wa Darfur, uhalali wa uchaguzi huo na kuwepo kwa udanganyifu. Kwa upande wake Rais Al-Bashir amesema uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa licha ya baadhi ya wapinzani kuususia.