Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa IAEA apongeza mkataba baina ya Urusi na Marekani kupunguza nyuklia

Mkuu wa IAEA apongeza mkataba baina ya Urusi na Marekani kupunguza nyuklia

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za atomic IAEA amepongeza mkataba uliosainiwa leo baiana ya Marekani na Urusi wa kupunguza silaha za nyuklia.

Mkataba huo mpya utachukua nafasi ya ule wa 1991 uliojulikana kama START. Rais Baraka Obama wa Marekani na Demitr Medvedev wa Urusi wameafikiana kupunguza silaha zao na uzalishaji wa nyuklia kwa theluthi moja ambayo ni asilimia 30% zaidi ya ilivyokuwa awali.

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Yukiya Amano amesema kupunguza ushiriki na idadi ya silaha za nyuklia ni hatua muhimu katika kuelekea kuwa na dunia salama na huru isiyo na silaha za nyuklia, ambayo itakuwa na matokeo mazuri katika juhudi za kupunguza nyuklia duniani.