Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yakabiliwa na utapia mlo unaohitaji msaada

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yakabiliwa na utapia mlo unaohitaji msaada

Utafiti wa karibuni unaonyesha kuwa kuna utapia mlo wa hali ya juu katika majimbo matano ya congo DRC. Utafiti huo umefanywa na serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Wizara ya afya ya Congo DRC inakadiria kuwa zaidi ya watoto nusu milioni walio na umri wa chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito zaidi ya milioni moja wahitaji msaada wa dharura wa kukabiliana na utapia mlo.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNICEFmjini Kinshasa Joyce Brandful wakati kiwango cha utapia mlo kwa ujumla kiko nchi nzima katika majimbo matano kuanzia kaskazini magharibi hadi kusini mashariki hali ni mbaya zaidi. Amesema ukosefu wa chakula unaathiri watu wengi.

Wataalamu wanamini kwamba sababu ya utapia mlo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imechangia wa vita, bei kubwa za chakula na mdororo wa kiuchumi ambao umeitikisa sekta ya madini magharibi na kusini mashariki mwa nchi hiyo.