Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM imesaidia kuwarejesha wahamiaji wa Ethiopia waliokwama Somalia

IOM imesaidia kuwarejesha wahamiaji wa Ethiopia waliokwama Somalia

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limewasaidia takribani wahamiaji wa Kiethiopia 500 waliokuwa wamekwama nchini Somalia kurejea nyumbani.

Waethiopia wapatao 11,000 wanaishi katika mji wa Bosaso kaskazini mwa Somalia na wengine wamekuwa hapo kwa miaka 15. IOM inasema operesheni ya kuwarejesha nyumbani kwa hiyari Waethiopia hao ilianza Machi 31 hadi April 4 na ilifadhiliwa na mkutano wa kimataifa wa Tokyo wa maendeleo ya Afrika.

Miongoni mwa mambo wanayoyapata wahamiaji hao wanaoondoka kwa hiyari ni kupimwa afya zao, usafiri na fedha za kuwasaidia kwenda kuanza maisha mapya. Na wakati mwingine wanapewa ushauri wa kazi na bishara ndogondogo.