Ban Ki-moon ahitimisha ziara Asia ya Kati na kuelekea Vienna Austria

Ban Ki-moon ahitimisha ziara Asia ya Kati na kuelekea Vienna Austria

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehitimisha ziara yake ya wiki moja Asia ya kati ambako alizuru nchi tano.

Katika ziara hiyo ya siku saba bwana Ban amezungumza na viongozi wa nchi hizo zote na kujadili masuala muhimu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Miongoni mwa masuala aliyoyasisitiza ni kuzingatia haki za binadamu, uhuru wa kuzungumza, demokrasia na kutatua mizozo kwa njia ya amani na majadiliano.

Leo bwana Ban ameelekea Vienna Austria ambako atakuwepo hadi tarehe 10 Aprili. Pamoja na mambo mengine atahudhuria kikao cha bodi ya wakurugenzi wa Umoja wa Mataifa. Pia atahutubia baraza la shirika la usalama na ushirikiano Ulaya OSCE.