Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi Sudan unaendelea kukumbwa na utata, SPLM sasa kugomea Sudan kaskazini

Uchaguzi Sudan unaendelea kukumbwa na utata, SPLM sasa kugomea Sudan kaskazini

Uchaguzi nchini Sudan unaotarajiwa kufanyika kuanzia mwishoni mwa wiki hii unaendelea kughubikwa na utata.

Baada ya vyama kadhaa vya upinzani kugomea uchaguzi huo chama kikubwa cha SPLM ambacho kimejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais sasa kinasema kinagomea uchaguzi wa bunge kwenye majimbo 10 kati ya 15 ya Kaskazini mwa Sudan.

Hata hivyo chama hicho kitaendelea kushiriki uchaguzi kwenye eneo la kusini ambako kina umaarufu mkubwa. Katibu mkuu wa SPLM Pagan Amum amesema hatua ya kususia ni kuonyesha kutoridhika na hali ya usalama kwenye jimbo la Darfur na hofu ya kuwepo wizi wa kura. Huu ni uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Sudan tangu mwaka 1986. Umoja wa Mataifa umesema utajitahidi kuisaidia Sudan kufanikisha azma ya uchaguzi huo.