Hali ya tahadhari imetangazwa Kyrgystan baada waandamanaji kuawa

7 Aprili 2010

Hali ya wasiwasi imeongezeka nchini Kyrgystan baada ya waandamanaji wanne kuuawa katika makabiliano na polisi mjini Bishkek.

Rais wan chi hiyo Kurmanbek Bakiyev ametangaza hali ya tahadhari na waandamanaji waliokuwa wamejaa nje ya offisi yake wamekuwa wakivurumishia mawe polisi. Kituo cha televisheni ya taifa cha nchi hiyo kimearifiwa kuvamiwa na sasa kuwa chini ya waandamanaji hao ambao wanamtaka Rais kujiuzulu kutokana na madai ya ufisadi na ongezeko la gharama za umeme na gesi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa taarifa kuhusu hali inayoendelea Kyrgystan na kusema ameshtushwa na umwagikaji damu uliotokea na amewaomba raia kuwa watulivu pia ametoa wito wa kufanyika mazungumzo haraka ili kutatua mzozo huo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud