Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani Congo DRC waokoa watu 29 waliokwama ziwa Kivu

Walinda amani Congo DRC waokoa watu 29 waliokwama ziwa Kivu

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo wamewaokoa watu zaidi ya 20 waliokuwa wakisafiri kwa boti kutoka Kivu baada ya injini ya boati hiyo kuzimika.

Walinda amani hao wanaojulikana kama MONUC jana waliwaopoa abiria 25 akiwemo naibu gavana wa Kivu ya Kusini Jean Paul Kibala na wafanyakazi wanne wa boti, baada ya boti iitwayo Amani kuzima kilometa 75 kutoka kijiji cha Kashofu kwenye ncha ya kusini ya ziwa Bukavu.

MONUC baada ya kupashwa habari walipeleka haraka wanajeshi na maafisa wa uokozi 25, boti mbili za doria na boti tatu za ukozi. Abiria hao walipelekwa kwenye kisiwa cha karibu cha Idjwi ambako walipanda boti nyingine. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo na wanajeshi hao wa kulinda amani kutoka Uruguay waliweza kuivuta boti hiyo na kutengeneza injini yake.