Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imesaidia kuandikisha wakimbizi wa Colombia walioko Equador

UNHCR imesaidia kuandikisha wakimbizi wa Colombia walioko Equador

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR chini ya mradi wake mpya limefanikiwa kuwaandikisha wakimbizi elfy 26 wa Colombia waliko kaskazini mwa Equador.

Kwa mujibu wa msemaji wa kamishina mkuu wa UNHCR Andrej Mahecic uandikishaji huo ni hatua muhimu katika kuelekea kutambuliwa rasmi kwa watu hao kama wakimbizi.Jopo la watu wanaojumuisha maafisa wa wizara ya mambo ya nje ya Equador na wafanyakazi wa UNHCR wamesafiri hadi maeneo ya ndani vijijini.

Katika uandikishaji huo waliotambulika kama wakimbizi rasmi walipewa vibali vya ukimbizi na ambao kesi zao zinahitaji kushughulikiwa walipewa karatasi za kuonyesha wanaomba hifadhi za ukimbizi.