Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wa Mali na Niger walioathirika na hali ya hewa kusaidiwa na ICRC

Wakulima wa Mali na Niger walioathirika na hali ya hewa kusaidiwa na ICRC

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu limeanza programu maalumu ya kuwasaidia watu zaidi ya lakini moja kaskazini mwa Niger na Mali.

Watu hao ni waliioathirika na msimu mbaya wa mvua ambazo hazikunyesha ipasavyo na kuleta njaa kubwa, na pia walioathirika na machafuko. Watu hao laki moja ni sehemu tuu ya mamilioni ya watu wengi ambao ni wakulima na wafugaji walioathirika na hali hiyo mbaya ya hewa na matatizo ya kiuchumi.

Mbali ya hayo mapigano ya kikabila yanayoendelea katika baadhi ya sehemu za nchi hizo yameongeza shinikizo kwa maisha ya watu. Maxwel Isad ni msemaji wa ICRC