Kesho ni kumbukumbu ya kimataifa ya miaka 16 mauaji ya kimbari ya Rwanda
Kesho Jumatano April 7 ni siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda yaliyofanyika 1994.
Hapa New York katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutafanyika hafla maalumu ya kuwakumbuka walioathirika na kuuawa katika mauaji hayo yaliyochukua siku 100.
Katika ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, na vituo vingine vya UM kote duniani kutakuwa kukionyeshwa filamu maalumu ya kumbukumbu hiyo ambayo sasa ni miaka 16.
Katika hafla ya New york itaambatana na burudani ya muziki kutoka kwa wanamuziki chipukizi wa Rwanda na hotuba ya naiabu Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Dr Asha Rose Migiro. Wengine watakaohutubia ni pamoja na mwakilishi wa kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Eugene Richard Gasana na manusura wa mauaji ya kimbari bi Jacqueline Murekatete.