Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Haiti wanarejea mashuleni miezi mitatu baada ya tetemeko la ardhi

Watoto Haiti wanarejea mashuleni miezi mitatu baada ya tetemeko la ardhi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF pamoja na washirika wake wanaunga mkono wito wa wizara ya elimu ya Haiti ya kuwataka watoto warejee mashuleni.

Wito huo umetolewa ikiwa ni chini ya miezi mitatu tangu nchi hiyo kukumbwa na tetemeko kubwa  la ardhi lilitikisa maisha ya familia na watoto wengi katika mji mkuu Port-au-Prince.

Wito huo ni hatua ya mwanzo ya operesheni inayotumai kushuhudia wanafunzi laki saba wakirejea mashuleni katika miezi miwili ijayo, na idadi inatarajiwa kuongezeka msimu mpya wa shule utakapoanza mwezi septemba.