Ban Ki-moon anahitimisha ziara asia ya Kati kwa kuzuru Kazakhstan

6 Aprili 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko nchini Kazakhstan katika kuhitimisha ziara yake ya Asia ya Kati.

Bwana Ban amewasili Kazakhstan akitokea Tajikstan ambako alijadili na viongozi wa nchi hiyo masuala mbalimbali likiwemo suala Afghanistan, haki za binadamu, mabadiliko ya hali ya hewa na suala la maji linaloleta mvutano baina ya nchi za Asia ya kati.

Kuhusu mvutano huo wa maji bwana Ban amesema mali asili ya aina yoyote ile iwe ni gesi, mafuta au maji, ni lazima itumike kwa usawa na kwa kuheshimu matakwa ya nchi majirani.

Akitoka Asia ya Kati Katibu Mkuu atelekea Vienna kuanzia April 7 hadi 10 ambako pamoja na mambo mengine atahudhuria kikao cha bodi ya wakurugenzi wa Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter