Skip to main content

Wanajeshi 2000 wa MONUC kupunguzwa Congo DRC ifikapo mwisho wa mwezi Juni

Wanajeshi 2000 wa MONUC kupunguzwa Congo DRC ifikapo mwisho wa mwezi Juni

Licha ya machafuko na ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo vikosi vya MONUC vitapunguzwa

Machafuko yanafanywa na pande zote waasi na jeshi la serikali. Serikali ya Congo imepiga hatua kubwa ikisaidiwa na wanajeshi 20,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na sasa inataka walinda amani 2000 wapunguzwe ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni.

Lakini Umoja wa Mataifa haukubaliani na tarehe iliyopendekezwa na serikali ya congo ya kutaka mwezi August 2011 iwe ndio mwisho wa vikosi hivyo kuwepo Congo baada ya MONUC kukaa nchini humo kwa miaka 11 . Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema katika ripoti yake kuhusu MONUC kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Congo imepiga hatua ukilinganisha na changamoto ambazo nchi hiyo imekabiliana nazo kwa miaka 15.

Hatahivyo amesema bado kuna changamoto zinazoikabili serikali ,ikiwepo mapigano ynayoendelea dhidi ya waasi katika majimbo ya Kivu ya Kaskazini na Kusini mashriki mwa nchi hiyo ambako kuna ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu , taasisi za serikali hazina nguvu, pia kuna haja ya kufanya mabadiliko katika jeshi la serikali, polisi na ambako hali ya maisha ni ngumu sana ikiwemo katika mji mkuu Kinshasa. Bwana Ban amelifuta pendekezo la serikali la kutaka vikosi vyote vya MONUC view vimeondoka ifikapo tarehe 30 August 2011.