Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya elimishaji na msaada kuhusu mabomu yaliyotegwa

Leo ni siku ya kimataifa ya elimishaji na msaada kuhusu mabomu yaliyotegwa

Leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha watu juu ya mabomu na kusaidia kuchukua hatua dhidi ya mabomu hayo.

Katika kuadhimisha siku hii shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa wito wa kuwepo na hatua zaidi za kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya athari za mabomu yaliyotegwa ardhini na vifaa vingine vinavyoweza kuripika ambavyo ni mabaki ya vita.

Naibu mkurugeni wa UNICEF Hilde F. Johnson amesema watoto wengi wanauawa kutokana na silaha hizo, japo amesema jumuiya ya kimataifa imepiga hatua kuelekea kufikia lengo la mkataba wa kupinga mabomu tangu ulipoanza kutumika 1999.

Ameongeza kuwa kila siku mamia ya watu wanajeruhiwa na wengine kuuawa kote duniani kutokana na mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vingine vya kuripuka vilivyosalia miaka mingi baada ya vita kumalizika.