Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa, ECOWAS na AU waingilia jaribio la mapinduzi Guinea-Bissau

Umoja wa Mataifa, ECOWAS na AU waingilia jaribio la mapinduzi Guinea-Bissau

Umoja wa Mataifa umesema unaunga mkono mpango wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi ECOWAS na Umoja wa Afrika AU kutuma ujumbe mkali kwa vikosi vya jeshi nchini Guinea-Bissau.

Ujumbe wa ECOWAS, AU na Umoja wa Mataifa uliwasili jana mchana nchini humo kufikisha ujumbe kwa vikosi vya jeshi kufuatia hatua yao ya siku ya Alhamisi iliyopita ya kumkamata mkuu wa majeshi jenerali Jose Zamora Induta.

Waziri mkuu wa Guinea-Bissau Carlos Gomes Junior pia alilazimishwa kukaa kwenye kifungo cha nyumbani na kupewa vitisho vya kuawa.