UNICEF yataka maji na usafi vidumishwe mashuleni kusaidia afya za watoto

UNICEF yataka maji na usafi vidumishwe mashuleni kusaidia afya za watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na washirika wake wamesema ukosefu wa maji salama na usafi mashuleni vinaathiri uwezo wa watoto kusoma na afya zao.

UNICEFU imeyasema hayo katika ripoti yake iliyozinduliwa leo ya kusafisha mikono, kusoma kwa bidii, afya na kushiriki katika kunawa mikono mashuleni.

Ripoti hiyo inasema katika nchi 60 zinazoendelea karibu zaidi ya nusu ya shule za msingi hazina huduma ya maji na theluthi mbili hazina vyoo. Ripoti hiyo imetolewa leo mjini Dubai kwa ushirikiano wa UNICEF na washirika wake.