Skip to main content

MONUC yalaani mauaji ya walinda amani huko Mbandaka DR Congo

MONUC yalaani mauaji ya walinda amani huko Mbandaka DR Congo

Wapiganaji wenye silaha wamewauwa wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa Kaskazini magharibi mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUC umesema waasi waliokuwa na silaha nzito wameushambulia mji wa Mbandaka na kuteka uwanja wa ndege ,pia kuuwa askari wa kulinda amani kutoka Ghana na mfanyakazi mwingine wa Umoja huo.

MONUC imelaani vikali mauaji hayo ambayo pia yamekatili maisha ya raia wengi. Hivi sasa MONUC na vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefanikiwa kuudhibiti tena uwanja huo.

Mapigano ya eneo hilo ni tofauti kabisa na machafuko yanayoendelea baina ya makundi yenye silaha Mashariki mwa Congo.

Makundi mawili ya kikabila Mbandaka yanazozania haki ya kuvua samaki.Mmoja wa wafanyakazi wa MONUC anafafanua kuhusu hali ilivyo.