Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waandishi wa habari watano wameuawa Honduras mwezi Machi

Waandishi wa habari watano wameuawa Honduras mwezi Machi

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kutetea uhuru wa vyombo vya habari leo limezungumza kupinga mauaji ya waandishi wa habari America ya kati.

Wiki iliyopita waandishi wawili waliuawa na hivyo kufanya jumla ya waandishi wa habari waliouawa Amerika ya kati kufikia watano kwa mwezi Machi pekee.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, Irina Bokova amesema ukatili huo dhidi ya waandishi wa habari unakandamiza uhuru wa habari na demokrasia katika jamii. Ameitaka serikali ya Hondurus kufanya kila juhudi kuwakamata wahusika na kuwachukulia hatua ili kukomesha mauaji hayo.