Homa ya bonde la ufa imeikumba Afrika Kusini watu wawili wafariki dunia

Homa ya bonde la ufa imeikumba Afrika Kusini watu wawili wafariki dunia

Wizara ya afya nchini Afrika ya Kusini imearifu kuwa homa ya bonde la ufa (RVF) imeingia nchini humo na kuua watu wawili.

Visa vingine 63 vya ugonjwa huo vimeripotiwa katika majimbo ya Free State, Estern Cape na Northen Cape.

Waathirika wengi inasemekana wamekuwa pamoja na mifugo iliyoathirika au mashamba ambayo yamethibitishwa kuingiliwa na homa hiyo.Wengi wa watu walioambukizwa homa hiyo ni wakulima, madaktari wa mifugo na wafanyakazi wa mashambani.

Waathirika wote wamethibitishwa kuwa na homa hiyo baada ya vipimo kuchunguzwa katika taasisi ya taifa ya magonjwa ya kuambukiza mjini Johanesberg. Kwa upande wa mifugo homa hiyo imekuwepo na inaendelea kuathiri kondoo, mbuzi, ng'ombe na wanyama wa porini, na mbali ya majimbo hayo pia majimbo mengine yaliyoathirika ni western Cape, Mpumalanga, na Gauteng.