Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanataka kuwepo na ulinzi kwa wahamiaji nchini Japan

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanataka kuwepo na ulinzi kwa wahamiaji nchini Japan

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki za wahamiaji Jorge A. Bustamante ametoa wito kwa serikali ya Japan kuongeza ulinzi kwa wahamiaji na familia zao.

Bwana Bastamante ametoa wito huo baada ya ziara ya siku tisa nchini Japan. Amesema wahamiaji bado wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ubaguzi wa rangi, kunyonywa, hali ya polisi na mfumo wa sheria kupuuza haki zao na kutokuwepo kwa sera maalumu ya kulinda haki zao za binadamu.

Wakati akiipongeza serikali ya Japan kwa baadhi ya hatua iliyozichukua kupunguza athari za kiuchumi kwa wahamiaji na familia zao, amesisitiza kuwa Japan bado haina sera maalumu inayolinda haki za wahamiaji, ikiwa ni miaka 20 tangu ilipoanza kupokea wafanyakazi wahamiaji.