Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon yuko ziarani Asia ya kati

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon yuko ziarani Asia ya kati

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameanza ziara ya wiki moja kuanzia leo Asia ya Kati.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky hii ni ziara ya kwanza ya Bwana Ban Asia ya kati tangu alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Ziara hiyo itajumuisha nchi zote za Asia ya kati akianzia Turkmenistan, kisha Kyrgyzstan,na baada ya hapo atakwenda Tajikistan na Uzbekistan na atamalizia ziara yake nchini Kazakhstan. Atazuru nchi zote hizo kwa wiki moja lakini amesenma ni ziara muhimu sana hususani katika eneo hilo kisiasa na kimaendeleo.