Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nusu ya watu wa Niger wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula

Nusu ya watu wa Niger wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula

Nusu ya watu wa Niger wanakabiliwa na matatizo makubwa ya chakula kutokana na mvua za masika kutonyesha na mavuno hafifu mwaka jana.

 Onyo hili limetolewa na mwakilishi mpya wa umoja wa mataifa nchini humo Khardiata Lao N'Diaye.

Bi N'Diaye amewaambia waandishi wa habari hapa New York kuwa dola milioni 150 zinahitajika kukabiliana na hali hiyo. Amesema Niger ina watu milioni 15 na nusu yake, milioni 7.8 wanakabiliwa na njaa. Na amesema mbali ya upungufu wa chakula na kuna utapia mlo hususani kwa watoto na kina mama wajawazito.


Bi N'Diaye ametanabaisha kuwa Umoja wa Mataifa na washirika wake wa misaada ya kibinadamu wameandaa mipango ya dharura ya kuisaidia Niger kwa matatizo hayo ya chakula.