Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umeonya kuwa ahadi za kupungua gesi ya viwanda hazitoshi kufikia malengo ifikapo 2020

UM umeonya kuwa ahadi za kupungua gesi ya viwanda hazitoshi kufikia malengo ifikapo 2020

Katibu mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa Yvo de Boer amesema ahadi zilizotolewa na nchi mbalimbali kupunguza gesi za viwandani hazitoshelezi kufikia malengo ifikapo mwaka 2020.

Amesema tangu kumalizika kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Copenhagen Denmark ahadi walizopokea za kupunguza gesi za viwandani ni 75 ambazo kwa jumla zinahusika kwa utoaji wa asilimia 80 ya gesi ya viwandani duniani.

Bwana de Boer amesema hii inaonyesha wazi kwamba wakati ahadi ni hatua muhimu kuelekea malengo ya kupunguza ongezeko la gesi ya viwandani ,pekee hazitoshelezi kufikia malengo ya kupunguza gesi hiyo hadi chini ya nyuzi 2 ifikapo 2020.