Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC imeridhishwa na kuachiliwa kwa mateka mwingine wa Colombia

ICRC imeridhishwa na kuachiliwa kwa mateka mwingine wa Colombia

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu ICRC, limesema limeridhika na limefurahishwa na kuachiliwa kwa Sajenti Pablo Moncayo.

Moncayo alitekwa na wapiganaji wa kundi la FARC miaka kumi na miwili iliyopita. Alikabidhiwa kwa ujumbe wa ICRC na seneta wa Colombia Piedad Cordoba jana jioni.

Hii ni mara ya pili operesheni kama hiyo ya kibinadamu inafanyika ndani ya wiki moja. Hatua hiyo imewezekana kutokana na juhudi za serikali ya Brazil, serikali ya Colombia na jeshi lake la ulinzi na polisi, wanaharakati wa kupigania haki wa Colombia, kanisa la nchi hiyo na kundi lenyewe la FARC. Moncayo aliweza kuonana na familia yake kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12.