Skip to main content

Mkutano wa wahisani kuisaidia Haiti umeanza leo mjini New York

Mkutano wa wahisani kuisaidia Haiti umeanza leo mjini New York

Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 130 leo wameanza mkutano katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York kwa lengo la kukusanya fedha za kuisaidia Haiti baada ya kukubwa na tetemeko la ardhi mwezi Januari.

Watu mbalimbali wanatoa mada kwenye mkutano huo waliouita "kuelekea mustakabali mpya wa Haiti" akiwemo Rais wa Haiti Rene Preval, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti Bill Clinton.

Mkutano huo unaongozwa kwa ushirikiano na Brazil, Muungano wa Ulaya Ufaransa na Hispania. Hasara iliyosababishwa na tetemeko la Januari 12 Haiti ni vifo zaidi ya 220,000 na kuwaacha watu wengine milioni tisa wakihitaji msaada. Kwa mujibu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP harasa iliyopatikana ni takribani bilioni saba.

Waziri wa mambo ya nje wa Haiti Jean-Max Bellerive atawasilisha mipango waliyonayo na mahitaji ya nchi yake . Na ndipo nchi mbalimbali, mashirika ya kimataifa na washirika wengine watapata fursa ya kuahidi msaada wao kwa ajili ya kusaidia ujenzi mpya wa Haiti. Katika ufunguzi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewashukuru wahisani waliofika mkutanoni.