ICC yatoa ruksa kufanyika uchunguzi wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya

ICC yatoa ruksa kufanyika uchunguzi wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoko The Hague Uholanzi leo limetoa ruksa kwa ombi la waendesha mashitaka kuchunguza uhalifu dhidi ya binadamu unaodaiwa kufanyika Kenya katika ghasia za baada ua uchaguzi mkuu miaka miwili iliyopita.

Watu wapatao elfu moja waliuawa katika machafuko hayo na wengine laki tatu walilazimika kukimbia nyumba zao. Mwezi Novemba mwaka jana mwendesha mashitaka Luis Moreno- Ocampo aliomba ridhaa ya kuanza uchunguzi dhidhi ya ghasia hizo za mwaka 2007 zilizotokana na utata wa matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Rais Mwai Kibaki dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga ambaye kwa sasa ni waziri mkuu.

Jaji Hans-Peter Kaul amesema kwamba uhalifu uliofanyika Kenya haujafikia hadhi ya kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu chini ya mkataba wa Roma ambao Kenya iliridhia mwaka 2005.

Amehitimisha kwamba hakukuwa na sababu za msingi kuamini kwamba uhalifu uliofanyika Kenya ilikuwa ni mashambulizi yaliyolenga dhidi ya raia au ilikuwa ni sera kutoka kwa serikali au shirika jambo ambali linahitajika katika mkataba wa Roma.