Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti inahitaji dola bilioni 11ili kujijenga upya katika miaka kumi ijayo

Haiti inahitaji dola bilioni 11ili kujijenga upya katika miaka kumi ijayo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo katika mkutano wa wahisani hapa New York amesema katika miaka kumi ijayo Haiti itahitaji dola bilioni 11 kujijenga upya baada ya tetemeko la ardhi la Januari.

Ban amesema kwa wiki kadhaa wataalamu wamekuwa wakitathimini mahitaji na gharama zilizosababishwa na tetemeko la ardhi nchini Haiti. Ameongeza kuwa Rais wa Haiti Rene Preval na maafisa wengine wa serikali wamekuwa wakiifanyikia kazi mipango ya kusaidia ujenzi mpya wa nchi hiyo.

Amesisitiza kuwa lengo sio tuu ujenzi mpya,bali ni kuifanya Haiti iwe bora zaidi, ambapo watu walio wengi wasiishi tena kwenye umasikini uliokithiri,ambapo hawawezi hata kwenda shule na kuwa na afya njema. Pia amesema wawe na uchaguzi kuliko kukosa ajira au kuondoka nchini.

Amemalizia kwa kusema katika mpango huu tume ya muda ya ujenzi wa Haiti itatoa dola bilioni 4 kwa ajili ya utekelezaji wa mipango hiyo na miradi mbalimbali katika miezi 18 ijayo.